LEO ni vita ya kufunga mwaka kwenye Ligi Kuu Soka ya Hispania maarufu kama La Liga, amabapo Miamba miwilli ya Soka Duniani Barcelona na Real Madrid kukutana kwenye mchezo wa ligi kuwania point 3 muhimu na kuweza kufunga mwaka kwa furaha kwa mashabiki wake.
Katka Mchezo huo ambao utachezwa kwenye uwanja wa Barcelona, Camp Nou unatarajiwa kurushwa na Jumla ya kamera 31 za mfumo wa HD 4K. Hii ni mara ya kwanza kwa mchezo mmoja kurushwa na kamera nyingi kiasi hicho. Itakuwepo pia kamera moja ikiwarekodi Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, muda wote.
nyota wawili hao Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Lionel Messi wa Barcelona watakuwa wanawania kufunga mwaka wakiwa na mabao mengi zaidi.
Kwasasa nyota hao wana mabao 53 kila mmoja ambayo wameyafunga ndani ya mwaka huu wa 2017 katika mashindano yote. Wanaingia kusaka mabao mengine ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kumaliza mwaka wakiwa na rekodi ya kuwa na mabao mengi zaidi.
Kwa upande wa viwango timu hizo zote zinafanya vizuri pamoja na Real Madrid kuanza vibaya msimu, tayari imeshaanza kurejea kwenye ubora wake haswa ikipewa nguvu na ubingwa wa klabu bingwa ya dunia ilioupata wikiendi iliyopita.
Kuelekea mchezo wa leo utakaopigwa saa 9:00 alasiri, Barcelona ndio vinara wa ligi wakiwa na alama 42 huku wakiwa wameruhusu nyavu zao kuguswa mara saba tu katika mechi 16 huku Real wakiruhusu mabao 11 katika mechi 15 na wakishika nafasi nne wakiwa na alama 31.
Mechi ya leo ni El Clasico ya 237 katika historia ya timu hizo. Real Madrid imeshinda mara 95 huku Barcelona ikishinda mara 92 na kutoka sare mara 49. Messi ndio mfungaji wa muda wote wa El Clasco akiwa na mabao 24 akifuatiwa na Alfredo Di Stefano mwenye mabao 18 na Ronaldo akiwa na mabao 17.