Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Wakati tukielekea kwenye uchaguzi Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), CP .Salumu Rashid Hamduni ,amevitaka vyombo vya habari na wadau mbalimbali nchini kushirikiana kupiga vita rushwa ili kupata viongozi bila kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Hamuduni ameyasema hayo juzi jiji Dar Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi na wa habari wakati akifungu warsha ya siku moja, iliyowakutanisha Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini kwa lengo la kujadili namna ya kuzuia na kupambana na Rushwa wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.
Amesema wahariri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali nchini washirikiane kujenga kuijenga Tanzania ambayo viongozi wake watapatikana bila kujihusisha na vitendo vya rushwa.
CP Hamuduni amesema wahariri na waandishi wa habari wanao wajibu wa kuwajuza wananchi athali za rushwa ,hususani katika uchaguzi ili kuzuia upatikanaji wa viongozi wasio waadilifu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na kutozingatia misingi ya haki ,Usawa,Uwazi,Uwajibikaji na Uzalendo.
’’Hivyo itazoofisha utawala bora na demokrasia ambapo baadhi ya wananchi wenye sifa za uongozi bora kushindwa kugombea au kuteuliwa ,kutochaguliwa kwa kutokuwa tayari kutoa hongo kusababisha uvunjaji wa amani kutokana na migogoro ya mara kwa mara ya kisiasa na kusababisha taifa kuendelea kugubikwa na rushwa na hupelekea Wananchi kukosa imani na serikali na hata machafuko na kusikitisha zaidi ni kuwa kudhalilisha utu kwa kufananisha samani ya mtu na hongo ,fedha nguo chakula anayopewa ili apige au asipige kura.
Takukuru ina imani kuwa madhara hayo yanaweza kuepukika pale tu tutakapoamua kwa nia moja kushiriki moja kwa moja katika warsha hii kwa kujadili na kuandaa mikakati kwa kuzibiti vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi ,ushiriki wetu unafaida kubwa kwa taifa jamii na mtu mmoja mmoja ambapo utasadia wananchi kuwa na uelewa mpana kuhusu madhara ya rushwa kwenye uchaguzi na kasha kuchagua viongozi bora na si bora viongozi.
Ushiriki wenu ni ishara ya wazi ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali kuzibiti vitendo hapa nchini husussani kwenye uchaguzi,kama mnavyofahamu mwaka huu 2024 kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa na mwakani 2025 kutakuwa na uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani
Amesema kuwa utekelezaji wa mpango mkakati wa kuzuia na kupambana na Rushwa wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025, utatekeleza baada ya kumaliza kukusanya na kuchakata maoni yaliyotolewa na wadau.
TAKUKURU inaamini kwamba Mwananchi ambaye ndiye mpiga kura akifahamu haki yake na kutambua thamani ya kura yake ,hato kubali kurubuniwa kwa hongo na kudhalilisha utu wake kwa kupokea rushwa ili amchague kiongozi asiyefaa au aache kugombea au kupiga kura .
Takukuru inatambua imani kubwa ambayo wananchi wanayo kwa vyombo vya habari imani ambayo imewafanya wawatumie kama sauti zao , kuwasilisha kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kero ya rushwa
Amesema kuwa suala hilo kwasasasa ni mtambuka na kwamba uchaguzi unahusu wadau wengi wakiwemo TAKUKURU Tume huru ya taifa ,Wagombea na Vyama vya siasa vilivyosimamisha Wagombea na ndiyo maana wame anza kukutana na wadau tofautu tofauti ili yale yanayowahusu kama taasisi wanayawekea utaratibu wa utekelezaji na yale yanayohusu taasisi zingine watatoa ushauri kwakua ni moja ya majukumu yao ni kushauri.
Takukuru inafahamu umuhimu wa wahariri wa habari kama wadau muhimu sana katika mapambano dhidi ya rushwa tunafahamu kuwa pamoja na kuwa wadau katika mapambano dhidi ya rushwa wajibu wakufanya ,Kuhakikisha mihimili mitatu ya dola nchini Serikali ,Bunge na Mahakama inatekekeleza majukumu yao kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
’’K uhabarisha na kuelimisha umma wa Watanzania kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo changamoto ya uwepo wa vitendo vya rushwa katika maeneo mbalimbali, ili wabadili mitazamo yao na kujua kuwa vitendo vya rushwa ni kosa la jinai na pia ni uhujumu uchumi.
Warsha hii ni muendelezo wa jitihada za serikali za kuzibiti rushwa katika chaguzi ambazo serikali inayoongozwa na mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,imeendelea kuzifanya ambapo mpaka sasa imechukua hatua mbalimbali za kuhakikisha kuwa uchaguzi ujao unakuwa huru na wa haki na usio gubikwa na vitendo vya rushwa’’amesema.
Mwakilishi kwa upande wa wahariri Mgaya Kingoba kutoka Glgazeti la habari leo amesema ni vyma TAKUKURU walivyotambua mchango wa vyombo vya habari katika mapambano dhifi ya rushwa kwa kuwashirikisha wahariri kutoa maoni yao.
Amesema kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kusadia taasisi hiyo kupitia kalamu zao na kuwataka waandishi, kutumia nafasi zao kuelimisha jamii madhara ya rushwa na namna ya kukemea vitendo hivyo.