Korea Kaskazini imesema Jumapili kuwa vikosi vyake vya kijeshi viko tayari kuanzisha mashambulizi dhidi ya Korea Kusini, hatua ambayo imeongeza shinikizo kwa taifa hilo pinzani.
Korea Kusini imekataa kuthibitisha iwapo ilituma droni hizo lakini ikaonya kuwa itaiadhibu vikali Korea Kaskazini ikiwa usalama wa raia wake utatishiwa.
Siku ya Ijumaa, Korea Kaskazini iliishutumu Korea Kusini kwa kurusha karatasi hizo kwa mara ya tatu mwezi huu na kutishia kuwa itajibu vikali ikiwa tukio hilo litajirudia tena.
Katika taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini hapo jana, wizara ya ulinzi ya nchi hiyo imesema kuwa jeshi lake lilitoa agizo la awali kwa vitengo vya kijeshi vya silaha pamoja na vingine karibu na mpaka na Korea Kusini kujiandaa kikamilifu kwa mashambulizi.