Wizara ya sheria ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema watu 102 wamenyongwa na wengine 70 wamepangiwa kupewa adhabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa jana, watu hao, wanaume wenye umri wa baina ya miaka 18 na 35, walikuwa majambazi wenye silaha, wanaofahamika kama Kuluna, na walinyongwa kwenye gereza la Angenga kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Watu 45 tano walinyongwa mwishoni mwa mwezi Disemba na wengine 57 walinyongwa ndani ya masaa 48 yaliyopita.

Shirika la habari la AP limeripoti kuwasili kwa ndege iliyobeba watu wengine 70 kwenye mji wa Angenga, ingawa serikali haijasema chochote kuhusu wafungwa hao.

Wizara ya sheria imesema kundi la tatu la wafungwa hao watanyongwa kama makundi mawili ya mwanzo. Hukumu ya kifo ilikuwa imefutwa tangu mwaka 1981, lakini ikarejeshwa tena mwaka 2006, lakini utekelezaji wake 2003.