Kocha aliyekuja nchini takribani siku mbili zilizopita, Razaq Siwa, amerejea kwao Kenya bila kufahamu hatua ipi ya mazungumzo wamefikia na Yanga.
Siwa ambaye ni kocha wa makipa, aliwasili nchini kisha kupokelewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Hussein Nyika, kwa ajili ya mazungumzo ya kuanza kazi na klabu hiyo.
Lakini mpaka sasa tangu atue nchini, Siwa amekwea pipa na kurejea tena kwao huku ikiwa haijafahamika wamefikia hatua ipi ya mazungumzo na mabingwa hao wa kihistoria katika Ligi kuu Bara.
Wakati Siwa akiondoka, kikosi cha Yanga kipo katika mwendelezo makali kuhakikisha kinaiangamiza Gor Mahia FC Jumapili ya wiki hii.
Yanga itakuwa inacheza na wababe hao wa Kenya katika mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa na kumbukumbu ya kulazwa mabao 4-0 huko Nairobi wiki jana.