Na Mwamvua Mwinyi, JammhuriMedia,Chalinze
Kiwanda cha kutengeneza Marumaru cha KEDA kilichopo Chalinze, mkoani Pwani, kimetoa Boksi 1,750 zenye thamani ya sh.milioni 46 ikiwa ni mchango kwa shule za sekondari za Jakaya Mrisho Kikwete na Miono High School zilizopo halmashauri ya Chalinze.
Akiwashukuru wahisani hao, Mbunge wa Jimbo la Chalinze ambae pia ni Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete amewaasa wananchi kutunza miundombinu ya elimu ili kudumisha shule hizo.
Alieleza, ushirikiano na wadau mbalimbali utachochea maendeleo katika kuboresha shule zetu.
Ridhiwani anasema , Serikali inafanya kwa uwezo wake mkubwa kutenga fedha za kujenga miundombinu mbalimbali Lakini kwa juhudi za wadau kuongeza ushirikiano wao itasaidia kusukuma maendeleo ya sekta ya elimu.