…..Wajenga madarasa, kisima cha maji na kukarabati mabweni

Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Pwani

KAMPUNI ya Kutengeneza chupa za glasi ya KIOO Limited imefanikiwa kukarabati mabweni ya shule ya sekondari Vianzi iliyoko Mkuranga Mkoa Pwani hivyo, kuchimba kisima cha maji na kutoa madawati kwa shule ya msingi Vianzi hivyo kuchangia jitihada za serikali katika maendeleo ya elimu nchini.

Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Afisa Tarafa wa Tarafa ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, Clement Maulid, wakati akizindua miradi iliyofadhiliwa na kampuni hiyo Kata ya Vianzi Wilaya ya Mkuranga.

Miradi hiyo ni pamoja na ukarabati wa mabweni ya shule ya sekondari Vianzi, ujenzi wa kisima, Kompyuta na ununuzi wa madawati na meza kwa walimu na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Vianzi wilayani Mkuranga.

Aliwashukuru wakazi wa Kata ya vianza na kijiji cha Vianzi na uongozi wa KIOO Limited kwa miradi hiyo muhimu ya maendeleo ambayo alisema itasaidia kuinua kiwango cha elimu.

“Kwa niaba ya Wilaya ya Mkuranga nawapongeza sana KIOO Limited tunatambua thamani kubwa ya miradi iliyofanyika na mmetimiza wajibu wenu wa kurejesha sehemu ya faida kwa wananchi na mmeonyesha mfano mkubwa kwa wawekezaji walioko Mkuranga, nyinyi mmekuwa kioo kweli,” alisema.

Picha mbalimbali KIOO Limited ikikabidhi miradi iliyotekeleza shule ya Sekondari Vianzi Mkuranga Mkoa wa Pwani

“Mimi mwenyewe ni shuhuda wa mambo ambayo KIOO Limited wamefanya, niliwahi kuwatembelea kwenye kiwanda chao walitualika na Mkuu wa Wilaya tukaona kazi ya mchanga unaotoka Vianzi unachofanya kule,” alisema.

Alisema mabweni yaa wanafunzi yalikuwa yamechakaa sana lakini kwa namna wanavyozikarabati wanafunzi watakuwa wanafurahia sana kukaaa bweninini.

Alisema hata madawati na meza ambazo zimetolewa na kampuni hiyo zimetengenezwa kwa ubora.

“ Nimeona walimu wamepewa meza na viti vya kisasa sana ni shuleya kwanza kupewa vitu vyenye ubora namna hii na mazingira hayo yanawatia moyo walimu wa shule na kuwapa motisha kufanyakazi nzuri zaidi,” alisema.

Naye Mshauri Mkuu wa KIOO Limited, Richard Msumule, alisema kampuni hiyo imeajiri wafanyakazi 576 tangu kuanzishwa na inazlaisha wastani wa tani 400 kwa siku na asilimia kubwa ya bidhaa zinauzwa nje ya nchi.

Alisema kampuni hiyo inatosheleza mahitaji ya viwanda vya ndani vinavyotumia bidhaa za chupa za glasi kama vile chupa za soda, bia na pombe .

Alisema katika kuunga mkono juhudi za serikali wanashiirikiana na kijiji cha Vianzi kuboresha huduma za kijamii na kwa kuzingatia umuhimu huo wanakabidhi miradi kwa shule ya sekondari, msingi na zahanati Vianzi.

Alisema kwa upande wa Sekondari wamefanikiwa kuchimba kisima kirefu na kuweka tenki la lita 10,000 za maji, kununua madawati 50 na viti vyake na kujenga darasa moja.

Alisema kwenye Zahanati ya Vianzi wamechimba shimo la maji taka na kuweka umeme kwenye wodi mbalimbali na wamemetoa kompyuta za kisasa kwa zahanati hiyo.

“Tuna imani miradi iliyokabidhiwa leo itapunguza tatizo kwa kiwango na kuwafanya wanafunzi kusoma bila kuchoka hivyo kuongeza ufaulu na kuboresha elimu tatizo la maji kwa shule ya sekondari itakuwa historia, tunaomba wadau wengine wapenda maendeleo wajitokeze kuunga mkono jitihada za serikali kuwaletea maendeleo wananchi wake,” alisema.