JamhuriComments Off on Kinana azuru kaburi la Hayati Rais Magufuli
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Komredi Abdulrahman Kinana, akiwa ameambatana na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko wamezuru na kufanya sala katika kaburi la Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli nyumbani kwake, Chato mkoani Geita.