Rais Mstaafu wa Tanzania na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewasilisha Ujumbe Maalum ambao ulipokewa na Waziri wa Nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Guinea ya Ikweta, Simeon Oyono Esono Angue, kwa niaba ya Rais wa nchi hiyo, Teodoro Obiang Nguema Mbasogo.

Uwasilishaji wa ujumbe huo ulifanyika katika ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje jijini Malabo tarehe 13 Aprili 2025.

Katika tukio hilo, Kikwete pia alitoa salamu za Rais Samia, akisisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano, mshikamano, na umoja ili kukabiliana kwa pamoja na changamoto zinazokabili Bara la Afrika na dunia kwa ujumla.