Wizara ya Afya ya Uganda inasema mtoto wa mwaka mmoja anashukiwa kufariki kutokana na Ebola katika wilaya ya kati ya Mubende siku ya Jumanne.
Alikuwa miongoni mwa watu kumi na moja waliowekwa karantini kufuatia kisa kilichothibitishwa cha mwanamume mwenye umri wa miaka 24, aliyefariki Jumatatu.
Lakini kifo cha msichana mdogo bado hakijathibitishwa kuwa kilitokana na Ebola, kwa sababu maafisa bado wanasubiri matokeo kutoka kwa sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa watu waliowekwa karantini.
Siku ya Jumanne, maafisa wa Uganda walithibitisha kuzuka kwa homa ya virusi ya Ebola katika kijiji cha wilaya ya Mubende, zaidi ya kilomita 150 kutoka mji mkuu Kampala.
Shirika la Afya Ulimwenguni linasema kuwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha takriban muongo mmoja kwa kesi ya Ebola kuthibitishwa nchini humo.
Hii ni mara ya tano Uganda kupata mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, mara ya kwanza ulikuwa mbaya zaidi mwaka 2000 na kuua watu 224, na mlipuko wa mwisho nchini ilikuwa mwaka 2018. Milipuko mingine ilitokea 2014 na 2017.