Uwanja ambao nguli wa soka wa Brazil Pele alicheza baadhi ya mechi bora zaidi za maisha yake pia utaruhusu watu kutoa salamu zao za mwisho siku ya Jumatatu na Jumanne.
Santos, klabu ambayo Pele alicheza huko Brazil, ilisema katika taarifa kwamba umma utaweza kutoa heshima zao za mwisho kwenye Uwanja wa Vila Belmiro, nje ya Sao Paulo. Pele, ambaye jina lake kamili lilikuwa Edson Arantes do Nascimento, alifariki Alhamisi baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu. Alikuwa na miaka 82.
Santos ilisema jeneza lililombeba bingwa huyo mara tatu wa Kombe la Dunia litaondoka katika hospitali ya Albert Einstein mjini Sao Paulo mapema Jumatatu asubuhi na litawekwa katikati ya uwanja.
Mazishi yatafanyika kwenye ukumbusho wa Necrópole Ecumênica, kaburi la wima huko Santos. Familia pekee ndiyo itahudhuria. Pelé ana nyumba huko Santos, ambako aliishi zaidi wakati wa uhai wake.
Serikali ya Brazil ilitangaza siku tatu za maombolezo.
Anasifiwa kwa kufunga mabao 1,281 katika rekodi ya dunia katika mechi 1,363 katika kipindi cha miaka 21 ya maisha yake, yakiwemo mabao 77 katika mechi 92 za nchi yake.
Mchezaji pekee aliyeshinda Kombe la Dunia mara tatu, akinyakua taji hilo mnamo 1958, 1962 na 1970, Pele alitangazwa kuwa mchezaji Bora wa Karne wa Fifa mnamo 2000.
Alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo na kibofu katika miaka ya hivi karibuni.
Pele alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye utumbo wake mnamo Septemba 2021 katika Hospitali ya Albert Einstein mjini Sao Paulo, baada ya uvimbe huo kugunduliwa katika vipimo vya kawaida.
Alirejeshwa hospitalini mwishoni mwa Novemba 2022