Na Mwandishi wetu–Jamhuri Media
Dar es salaam

Naibu katibu Mkuu bara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Amani Golugwa, amesema kuwa kesi inayomkabili Tundu Lissu haiwezi kuchukuliwa kama vita dhidi ya wananchi, na akasisitiza kuwa wanachama pamoja na umma wana haki ya kufuatilia mwenendo wake.

Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 25, 2025 katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Mikocheni, Dar es Salaam, Golugwa amesema kuwa hawatakubali kesi hiyo kufanyika gizani.

“Kesi ya Lissu siyo vita Wananchi wana haki ya kujua kinachoendelea. Hatutakubali kesi hii kufanyika gizani,” amesema Golugwa.

Kauli hiyo imekuja wakati ambapo wanachama wa CHADEMA wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi hiyo, ambayo imeibua mijadala mbalimbali kuhusu haki, uwazi na demokrasia nchini.