Na Isri Mohamed

KESI inayomkabili ‘Afande’ Fatma Kigondo, imeahirishwa kwa maelezo kuwa bado haijapangiwa hakimu wa kuisikiliza, baada ya Hakimu Kishenyi aliyekuwa anaisikiliza awali kuhamishwa.

Taarifa hiyo imetolewa na Wakili Peter Madeleka wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema baada ya kuona tarehe waliyopangiwa na mahakama ya kusikiliza shauri hilo imepita, waliamua kufanya ufuatiliaji kwa Hakimu Mfawidhi Dodoma ili kujua nini kinaendelea.

“Katika hali ya kusikitisha tumeambiwa kwamba shauri litahairishwa mbele ya hakimu mwingine kwa sababu hakimu anayetakiwa kusikiliza shauri hili mwanzo hadi mwisho bado hajapangiwa, na hii inatokana na hakimu aliyekuwa analisikiliza shauri hili mheshimiwa Kishenyi kuhamishiwa mkoa wa Songwe”

“Mahakama ndio chombo cha utoaji haki, si chombo cha ukwamishaji haki, mahakama haipaswi kuchelewesha haki kupatikana kwa sababu zozote zile ambazo sio za msingi, sasa imechukua mwezi mzima tangu shauri hili lilipohairishwa Septemba 05, 2024 ili kurudi leo hapa, lakini tulichokuja kuambulia ni kwamba mahakama bado haijampangia hakimu mwingine”

Wakili Madeleka ameonesha kusikitishwa na kuilalamikia Mahakama kwa kuichelewesha haki ya mteja wake Paul Kisabo kupatikana kwa wakati.

Please follow and like us:
Pin Share