Leo Jumapili Machi, 4 2018 yamefanyika mashindano ya riadha mkoani Kilimanjaro ambayo ni maarufu kwa Kili Marathon ambayo hufanyika kila mwaka.
Mashindano haya hushirikisha watu kutoka mataifa mbalimbali, ambapo wale wote ambao hufanya vizuri hupewa zawadi, wakati wengine hupewa medali ikiwa ni ishara kwa walishiriki mbio hizo.
Mashindano haya yalianza mwaka 2003 yakiwa na washiriki waliokadiriwa kuwa kati ya 300-400 lakini sasa yamekuwa yakishirikisha maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali.
Katika mashindano hayo, raia kutoka Kenya wamekuwa wakifanya vizuri zaidi, na hata mwaka huu wamedhihirisha hilo baada ya kuongoza kwa kuwa na washindi wengi zaidi katika kilomita 21 na kilomita 42.
Hapa chini ni orodha ya washindi wa kilomita 21.
- Geofry Torotich- Kenya
- Simon Muthoni- Kenya
- Shadrack Korir- Kenya
- Daniel Kemoi- Kenya
- Stephen Mwendwa- Kenya
- Nicolas Kosgei- Kenya
- Tom Mutie- Tanzania
- Vincent Kimutai- Kenya
- George Njoroge- Tanzania
- Alex Bartilol- Kenya
Walioongoza katika kilomita 42, wote ni wawakilishi kutoka Kenya.
- Cosmas Muteti- Kenya
- Elkana Yego- Kenya
- George Onyancha- Kenya
- William Koskei- Kenya
- Kipngetich Timbwol- Kenya
- Francis Nzyoki- Kenya
- Stephen Kimbomet- Kenya
- Stephen Cimemin Njogu- Kenya
- Evans Taiget- Kenya
- Mark Lukuya- Kenya
Kwa mwaka 2019, mbio hizo zinatarajiwa kutimua vumbi Jumapili Machi 3, 2019.