Nasikitika vijana kukosa kazi
Ninasikitika kuona vijana wengi wasomi hapa Tanzania wakikosa kazi kwa muda mrefu baada ya kuhitimu masomo. Mikopo inayotolewa hairudishwi kwa wakati kwa sababu vijana hawana vyanzo vya mapato. Hivyo serikali itutafutie ufumbuzi wa tatizo hili kwa kasi, nguvu na ari mpya ili maisha bora kwa kila Mtanzania yapatikane.
Salim Habib, Morogoro
0652 054 343
JWTZ pumzikeni kwa amani
Askari wa JWTZ mliokufa kishujaa mkilinda amani nchini Sudan pumzikeni kwa amani. Natoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa wapiganaji hao. Ninaomba hayo malipo ya Sh milioni 100 yawafikie walengwa, hasa wajane na watoto wa askari hao, angalao yanaweza kuwasaidia.
Anko Mgingi Mhochi, Musoma
Serikali yetu ikubali kukosolewa
Viongozi wengi wa serikali ni wazushi, na wanataka kusifiwa siku zote, wanapokosolewa huanza kusingizia magazeti kwamba yanaandika uongo na kukipendelea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Mimi nawashauri viongozi wa aina hiyo wawe wanakubali kukosolewa.
Aziz Msafiri, Dodoma
0757 100 079
Viongozi kuweni na huruma
Viongozi mliokabidhiwa dhamana ya kuhudumia wananchi muwe na huruma. Mmeshindwa kupeleka walimu wenye vipaji katika Shule ya Sekondari ya Ngarenaro iliyopo kata ya National Housing. Naomba mshughulikie tatizo hilo jamani.
Mwananchi, Arusha
0756 253 900
Halmashauri Bariadi inanyanyasa watumishi
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi imekithiri vitendo vya ukiritimba, rushwa na upendeleo katika utoaji wa ruhusa kwa watumishi, hasa walimu wanaohitaji kwenda kujiendeleza kielimu na kitaaluma. Mkurugenzi na Afisa Elimu katika halmashauri hii ni kikwazo kikubwa.
Msomaji wa JAMHURI, Bariadi
0716 138 159
Watanzania tufungue macho tuone
Watanzania tunapaswa kufungua macho tuone jinsi wabunge wetu wengi wasivyowajali wapigakura, badala yake wamekuwa viongozi wa kushabikia mambo yanayowakandamiza wananchi, badala ya kutetea maslahi ya umma.
Mpenzi wa JAMHURI
0754 516 966
Nimeona taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa ndugu Samuel Sitta anahoji uhalali wa Lowassa kupita kwenye nyumba za ibada. Najiuliza maswali haya: (a) Anahoji kama nani? (b) Anahoji kwa nia gani? (c) Yeye ni msafi kwa kiwango gani mpaka ahoji wengine?
Msomaji
0752 633 555
Taifa langu. Taifa ambalo mabinti wakimwona Mzungu wanadhani ana hela, taifa ambalo ukiongea Kiingereza unaonekana umesema sana, taifa ambalo ukiwa na simu nzuri we mjanja japo vocha unaweka jerojero, taifa ambalo waliofeli wanakuwa walimu/polkisi, taifa ambalo mtu kwao hawana umeme ila analalamika Tanesco wanaboa, taifa ambalo warembo wameshaona wao ni wa kupewa daima, taifa ambalo vijana wanalalamika hawana, ukimpa dili anaanza longolongo, taifa ambalo ukiwa na gari hutongozi ukitoa lifti tu baaaas, taifa ambalo mwanafunzi anafaulu huku hajui kusoma wala kuondika. Nalipenda taifa langu.
0712 813285