JAMHURI linatufaa kuhusu JWTZ
Hakika ni ukweli usiopingika kuwa habari zinazochapishwa kwenye Gazeti Jamhuri kuhusu vikosi vya askari wetu wa JWTZ wanaolinda amani nchini Congo zimekonga mioyo yetu na zimetuongezea shauku ya kulipenda jeshi letu, hasa sisi tuliopo mpakani na Congo. Endeleeni kukaza buti katika kutujuza habari na makala motomoto, tuko pamoja.
Kamazima Kyaruzi, Kigoma
0752 333 487
Namuunga mkono Magufuli
Ninampongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli, kutokana na utendaji kazi wake mzuri unaozingatia maslahi ya taifa. Ninampongeza sana kiongozi huyo kutokana na msimamo wake imara katika Wizara ya Ujenzi. Mwenyezi Mungu azidi kumbariki siku zote.
Bernard Kilala, Geita
0755 818 975
Mungu wabariki wana JAMHURI
Ninawapongeza waandishi wa Gazeti Jamhuri kutokana na ushirikiano mlioonesha katika kuandaa gazeti hili kwani siyo kazi ndogo, Mungu awabariki. Endeleeni kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na ushirikiano bila kutegeana wala kutofautiana kimaslahi. Gazeti hili liko kwenye soko, tena najua ninyi ni wasomi makini, msiangushe taifa na sisi wasomaji wenu.
C.M. Nyakwar Otwalo, Shirati – Rorya
0784 668 841
Serikali iboreshe makazi Dar
Nadhani Serikali iboreshe makazi ya watu katika maeneo ya Kinondoni, Tandale, Manzese, Mikocheni, Vingunguti, n.k. kwa kutenga eneo la Mabwepande kwa ajili ya kujenga makazi ya kisasa na kuwahamishia huko wakazi wa maeneo niliyoyataja hapo juu kupisha ujenzi wa makazi ya kisasa kwa ajili ya kuwapangisha wananchi ili kujiongezea kipato na kupunguza tatizo la ukosefu wa makazi bora jijini Dar es Salaam.
Daniel, Kinondoni – Dar es Salaam
0658 313154
Zitto, Dk. Kitila wameonewa
Napenda kutoa ushauri kuhusu kutofautiana kwa viongozi wa CHADEMA. Ukisoma utete wa Kabwe Zitto na Dk. Kitila kuhusu waraka wa kufanya mabadiliko ya uongozi ndani ya chama, hiyo siyo uhaini wala kukisaliti chama, mimi nawaunga mkono. Ninamshangaa mwanasheria wa wa chama hicho Tundu Lissu, kwani hajaonesha uweledi katika hili bali ameonesha ushabiki wa upande mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu. Hajatenda haki. Marando Mabere hebu okoa CHADEMA.
C.M. Nyakwar Otwalo, Shirati – Rorya
0784 668 841
Lowassa okoa elimu Tanzania
Ni dhahiri kwamba katika Uchaguzi Mkuu ujao (mwaka 2015), Waziri mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, ndiye chaguo la Mungu, ingawa alidharauliwa, alitukanwa na kutemewa mate. Kwa kweli aliumia sana, ila ninamwomba atakapoingia katika ufalme wake asilipize kisasi, bali awasamehe bure watu wote walioshiriki kumwonea na kumuudhi, na zaidi awe hodari na mwenye moyo wa ushujaa.
Msomaji wa JAMHURI
0788 363 891
Serikali iache uonevu huu
Kwanini Serikali inashindwa kuweka mipaka katika maeneo ya wazi ili wananchi wasiyamavie na kujenga makazi. Ajabu ni kwamba Serikali hushtuka baada ya miaka mingi tangu watu walipovamia na kujenga makazi, hivyo kuwabomolea! Je, huo ndio utawala bora? Wakazi wa kijiji cha Kabange mkoani Katavi wamekubwa na tatizo hilo. Huo ni unyanyasaji unaotokana na uzembe wa Serikali.
Malimi Ng’halanga, Tumaini – Katavi
0782 356 435
Lowassa ukoe elimu Tanzania
Wakati Mheshimiwa Edward Lowassa akiwa Waziri Mkuu wa Tanzania, alisimamia vizuri mpango wa elimu ikiwa ni pamoja na kusimamia ujenzi wa shule za sekondari katika kila kata hapa nchini. Ni dhahiri tungekuwa tumepiga hatua kubwa sana katika elimu kuliko ilivyo sasa, ambapo elimu inadinimia! Mheshimiwa ninakuomba Lowassa okoa elimu Tanzania. Mungu akubariki.
Msomaji wa JAMHURI
0788 363 891