Itakuaje magaidi wakituingilia?

Mimi najiuliza sana kuhusu utendaji wa serikali yetu juu ya usalama wa taifa letu. Kama wauza dawa za kulevya wana uwezo wa kuviweka mfukoni mwao vyombo vya dola kama Polisi, Mahakama, DCI, DPP na Uhamiaji. Je, siku magaidi wakianza kuwatumia, nchi itakuwaje?

Magutu, Nyamongo – Tarime

0752 469 159

Rais Kikwete zinduka

Wakati umefika mafisadi wasambaratishwe. Nchi hii haitakuwa na uchumi thabiti hadi mtandao wa mafisadi utakapodhoofishwa. Mafisadi ni mojawapo ya ugaidi. Mafisadi wanaelekea kuteka karibu vyombo vyote vya dola hapa nchini! Rais Kiwete zinduka kabla nchi haijawa ngome ya mafisadi Afrika Mashariki.

 

Mpenda amani, Monduli – Arusha

0787 683 360

 

Samuel Sitta ananichanganya

Kauli za Sitta kuikosoa OPS Kimbunga na kutoa mfano wa ahadi za Rais kutotekelezeka kama mchumba anayetenda tofauti baada ya kuolewa, katika hotuba yake kwa wanavyuo mkoani Mbeya, binafsi namwona ni opportunist mpenzi wa madaraka na mnafiki. Kwanini chama chake kisimfukuze?

 

Kessy, Kibamba – DSM

0787 624 331

 

Tujihadhari Al-Shabaab wasituteke

Watanzania wenzangu, kwa muundo huu wa kikundi cha wanamgambo cha Al-Shabaab kuweza kupenya mpaka kwenda kuvamia, kuua na kuteka watu katikati ya Jiji la Nairobi, Kenya kuna uwezekano wa kusikia siku moja wameteka Ikulu hapa Afrika.

 

Maheri Maheri, Kahama – Shinyanga

0785 880 350

 

Tanzania tujihadhari na M23

Ninaomba kukumbusha kuwa yaliyotokea katika maduka makubwa ya biashara Westgate jijini Nairobi, Kenya yawe fundisho kwa Serikali ya Tanzania, kwani kwa mtazamo wangu, yaliyotokea huko yameelezwa ni malipizi ya Al-Shabaab. Nasi tusisahau kuelekeza macho kwa M23 wasije wakatuteka.

 

Negro man, Dar es Salaam

0765 441 474

Uchafu tishio wilayani Magu

Kwa sasa hivi Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, inaelekea kukithiri kwa uchafu wa mazingira, hasa katika maeneo yanayozunguka mnada ulio jirani na mjini, hakuna choo wala bafu, ingawa mamlaka husika imepandisha kiwango cha ushuru na maelfu ya watu wanatumia mnada huu!

 

Daniel Erasto, Mwanza

0756 378 940


Kondoa hatusomewi mapato

Wananchi katika Kikiji cha Magambu wilayani Kondoa, tunachangishwa fedha na serikali ya kijiji na kata kwa ajili ya maendeleo, lakini hautusomei mapato na matumizi ya fedha hizo. Tukiuliza tunatishwa kushtakiwa. Tulishamwambia mbunge wetu, lakini hajachukua hatua, tunaendelea kunyanyaswa!

 

Wananchi, Kondoa Kusini

0783 868 660

 

JAMHURI mmethubutu, hongereni

Hongereni wana JAMHURI, mmethubutu kuonesha maovu yanayofanyika katika nchi yetu. Siyo kazi rahisi ukizingatia vitisho mnavyopewa. Mfano mzuri ni ile orodha ya wauza ‘unga’ mliyofichua, ingawa bado haijafanyiwa kazi. Endeleeni kufichua maovu na Mungu atawasaidia katika kazi yenu. Sisi tupo pamoja nanyi.

 

Mathias Rwegasira, Dar

0787 918 384