Pongezi wana JAMHURI
Nawapongeza wafanyakazi wa Gazeti Jamhuri kwa kuanika wazi majina ya wauza unga katika toleo lililopita. Lakini kwanini serikali yetu isiwatie kitanzini kama huko China? Pia si hao tu, mafisadi nao watunguliwe risasi wazi wazi iwe fundisho kwa wengine wenye nia ya kufanya uovu huo.
Justus Julius Mwombeki, Bukoba
0753 191 029
Tuchangie maendeleo ya nchi
Hivi ni nani anawajibika kuchangia maendeleo ya nchi yetu Tanzania? Maana kila jambo likipitishwa linapingwa. Baadhi ya wanahabari badala ya kuhamasisha wananchi kuchangia maendeleo ya nchi yao wao kazi yao ni kuwakatisha tamaa. Hivi tunatoa fundisho gani kwa watoto wetu?
Mpenzi wa Jamhuri
0755 870 957
Wanahabari msiijibie serikali
Ni vema serikali ikajibu hoja za Jumuiya na Taasisi za Kiislam, badala ya ninyi [wanahabari] kuwa wasemaji wa serikali. Bila hivyo, tambueni kuwa kuandika/kujibu kwenu hakumalizi/hakufuti msamiati huo wa mfumo Kristo kwa sura moja tu ya kila anayesemwa dini yake kuwa na jicho la chongo.
Msomaji wa JAMHURI
0715 478 322
Unyama utaisha lini Tanzania?
Unyama utaisha lini. Huyo mfanyabiashara Mesenja Mayanda anaziamini sana pesa zake au kaiweka serikali mfukoni mwake ndiyo maana anajichukulia sheria mkononi?. Pole mzee Damas Masasila kwa kubomolewa nyumba zako na kuachwa bila makazi wewe na familia yako ya mke na watoto huko Geita.
Emmanuel Tungu Mashala, Igunga
0757 289 362
Mipango mingi isiyotekelezeka
Tanzania imejaliwa kuwa na watendaji wenye mipango lukuki isiyotekelezeka, hata inayotekelezwa siyo kwa asilimia zote, mfano tumeambiwa wauza unga ni vigogo walioko hata serikalini na wengine wametajwa kwa majina, lakini mbona katika hao waliotajwa na hili gazeti hatuwaoni hao viongozi?
Heze, Mwanza
0769 316 154
Serikali idhibiti dawa feki
Kwanini nchi yetu ya Tanzania yenye Serikali, Mamlaka ya Dawa na Chakula (TFDA), Polisi, Jeshi mipakani, mbwa na farasi wanaotengewa bajeti ya mamilioni ya fedha kila mwaka, lakini unaambiwa kuna DICLOFENIC feki mitaani? Dhamana ya maisha yetu iko kwa nani?
Mkereketwa wa Tanzania
0784 504 089
Serikali iisaidie familiya hii
Ndugu Mhariri, pole kwa kazi. Nimesoma habari ya unyama unaodaiwa kufanywa na mfanyabiashara Mesenja Mayanda na ofisa mtendaji kwa kubomoa makazi ya mzee Damas Masasila na familia yake wilayani Geita. Kwanini serikali inaacha wananchi wanyonge wanateswa kiasi hicho?
Raia mwema
0754 960 096