Wanahabari tembeleeni pia vijijini
Waandishi wa habari jaribuni kutembelea pia na maeneo ya vijijini kwa sababu huko kuna matukio mengi ya kutisha na kusikitisha, lakini vyombo vya habari vimekuwa havielekezi nguvu kubwa vijijini kama vinavyofanya maeneo ya mijini.
Obe Mlemi, Mugumu – Serengeti
0768 235 817
Watanzania tujihadhari na Rwanda
Watanzania tuweni macho kwani Wanarwanda hawatutakii mema, ndio maana rais wao anamkejeli Rais weu, Jakaya Kikwete, na hicho ni kijicho chao kwetu kutokana na amani iliyojengeka nchini kwetu. Wengine wanapenda kuona machafuko yanatokea Tanzania kama ilivyo katika nchi zao.
Baraka Chuma, Lindi
0788 736 736
Pongezi kwenu wana Jamhuri
Tunalipongeza Gazeti la Jamhuri kwa kutupatia habari motomoto, za kweli na zilizofanyiwa utafiti wa kina. Ushauri wangu kwa wabunge: Futeni kodi ya simu za mkononi, mbona mnataka kutuumiza kwa manufaa yenu wakati tumewachagua mkatuwakilishe bungeni tupate unafuu wa maisha.
Dk. Michael Hengele, Igunga
0713 600 741
Wakurya wavamia viwanja Msogora
Kuna watu wa jamii ya Wakurya huko Msogora, mtaa wa Taban, wanavamia viwanja, ukiwauliza wanasema kwamba wanaovamiwa wakaseme popote, wamejihami kwa silaha za jadi. Vitendo hivyo si vizuri, naomba serikali ilitambue hilo kwani linaweza kuzusha vurugu kubwa.
Msomaji wa Jamhuri
0754 025 726
Hongera JK kuwarejesha Wanyarwanda
Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, hongera kwa uamzi wako mgumu na sahihi juu ya kuwarejesha Wanyarwanda na Warundi katika nchi zao. Ila ukae ukijua kuwa uongozi wa Mkoa wa Kagera ni tatizo kwani haudhibiti wakimbizi wanaotwaa maeneo wilayani Karagwe. Mungu akulinde JK.
Maheri Maheri, Kagera
0785 880 350
Makala imebaini tatizo serikalini
Makala iliyochapishwa kwenye safu ya Fikra ya Hekima katika Gazeti la Jamhuri Agosti 6-12, 2013 yenye kichwa cha habari, “Viongozi hawa hawatufai”, imebaini hali ilivyo kwenye ofisi za umma. Kiini cha tatizo ni upendeleo katika uteuzi wa viongozi serikalini. Siku zote uswahiba uko katika misingi ya maslahi binafsi.
Henry
0755 446 670
Tuwakatae viongozi wasiojali watu
Watanzania wanapaswa kufungua macho waone viongozi wakiwamo mawaziri na wabunge wasiowajali wapigakura wao na Watanzania kwa jumla. Wabunge wamebaki kuwa watu wa kugonga meza kushabikia kila kitu kinachopelekwa na serikali badala ya kupigania maslahi ya wananchi.
Mwananchi mzalendo
0754 516 966
Wanahabari waibane CCM ibadilike
Hongera sana Gazeri la Jamhuri kwa makala zenye uchambuzi makini. Waandhishi wa habari mkiwa na msimamo wa kukibana na kukikosoa chama tawala – Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitabadilika na kutambua wajibu wake wa kuwatumikia Watanzania kwa uzito unaostahili.
Mwl. M. Nkya
0757 583 747