Meneja wa QNET, Muqtadir Suwani akizungumza na waandishi wa habari 
 Meneja wa QNET, Muqtadir Suwani(kulia) akipeana mkono na Katibu wa  kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha New Life Orphans Home, Hamadi Kondo mara baada ya kutoa msaada wenye thamani ya zaidi ya milioni Tsh.9/- kwa kituo hicho kilichopo Boko jijini Dar es Salaam jana. 
 Meneja wa QNET, Muqtadir Suwani(wa tatu kutoka kushoto waliosimama nyuma) akiwa na mawakala huru wa kampuni ya QNET Tanzania mara baada ya kutoa msaada wenye thamani ya zaidi ya milioni Tsh.9/- kwa kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha New Life Orphans Home kilichopo Boko jijini Dar es Salaam jana.

QNET inaleta Faraja kwa jamii zisizojiweza katika nchi 13 za kiafrika

· Kampuni hii inaleta furaha kubwa katika kituo cha kulelea watoto cha New LifeOrphans Home jijini Dar es salaam

Dar es Salaam, Mei 26 2018 – QNET, kampuni ya mauzo ya moja kwa moja inayoongoza kwa kushirikiana na mwakilishi wake wa kijitegemea (IRs) kuleta shangwe na faraja kwa jamii mbalimbali zisizojiweza katika kuashiria mwezi mtukufu wa Ramadhan, katika nchi 13 za Kiafrika.

Kampeni hii ya mwaka ina lengo la kuboresha maisha ya wengi na inaenda sambamba na falsafa ya kampuni hii ya (RYTHM) Jiinue kuwasaidia wanadamu (Raise Yourself to Help Mankind) Mafunzo ya msingi ya (RYTHM) wakati wote yamekuwa yanalenga katika kuongeza juhudi zaidi ya wajibu katika kujali wale ambao hawana uwezo kwa kuwapatia mazingira mazuri ya kuishi kwaajili yao, hasa watoto ambao ni alama ya kizazi chetu kijacho.

Kampeni ya mwaka huu ya Ramadhan katika Afrika itashuhudia ushirikiano mkubwa miongoni mwa wafanyakazi wa QNET, wakala na Wawakilishi Binafsi (IR) wakiunganisha jitihada zao katika kuandaa mfululizo wa mwezi mzima wa shughuli za kutoa misaada katika nchi kama Ivory Coast, Togo, Cameroon, Guinea, Burkina Faso, Tanzania, Niger, Uganda, Chad, Mali, Ghana and Senegal.

Nchini Tanzania, tukio la utoaji wa misaada ya Ramadhan litashuhudia utoaji wa mchele, tambi, sukari na bidhaa zingine za chakula na matumizi kwa kituo cha Kulelea watoto yatima cha New Life Orphans Home jijini Dar es salaam yenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 9/-.

Kuna watoto 105 katika kituo cha kulelea watoto yatima cha New Life Orphans Home ambacho kilianzishwa katika mwaka 2002. Makazi haya ya watoto kwa sasa yanasimamiwa na Mwanaisha Ahmed Magambo na wanategemea misaada ya umma na wasamaria wema kuweza kukabiliana na gharama za mahitaji ya watoto ya vyakula na vinywaji.

Akizungumzia kuhusu tukio hilo mwaka huu, Meneja wa QNET Muqtadir Suwani, amesema “Kampeni za kutoa misaada ya Ramadhan imekua moja kati ya kampeni zetu za msingi za kila mwaka. Kwa kweli ni muhimu sana, inatia moyo na inakamilisha jitihada za QNET. Kampeni kama hizi huhamasisha uwezeshaji wa jamii na pia huwa zinahamasisha sana kwa wafanyakazi wetu na Wawakilishi wetu binafsi (IR’s) kwa kushiriki wao binafsi katika kuboresha maisha ya wengine.

Hii ni kati ya falsafa ya QNET ya kuwezesha wajasiliamali kujiwezesha na kusaidia jamii.

Katibu wa kituo cha New Life Orphans Home bw. Hamad Kondo alisema “ Tunawashukuru kampuni ya QNET Tanzania kwa msaada huu ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa watoto wetu na naomba wafadhili wengine waige mfano huu.”