Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) Kinondoni kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo katika kipindi cha miezi miatatu Oktoba hadi Desemba 2023 imefanya uchunguzi kwa muda wa siku sita na kuthibitisha Kampuni ya PREZIDAR watendaji wake kuhujumu Mapato ya serikali kwa kuwasilisha benki kiasi kidogo kuliko uhalisia wake .
Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Takukuru Kinondoni
imebaini Kampuni Ismail Seleman amesema watendaji hao wamekuwa wakihujumu Mapato kwa kutotumia POS Mashine ipasavyo hivyo mnamo Januari 10 ,2024 watendaji hao walishtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni kwa tuhuma za uhujumu uchumi , ubadhilifu kusaidia kutenda kosa kuongoza genge la uhalifu na uchepushaji wa mapato ya ushuru ambapo makosa hayo kufunguliwa kesi Na 1638/2024.
“Takukuru kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi ya Manispaa ya Kinondoni tumefanya ufuatiliani na kubaini Kampuni hii iliyopewa jukumu la.kukusanya Ushuru wa Masoko ya Manispaa hiyo imekuwa ikifanya udanganyifu katika ukusanyaji na uwasilishaji wa mapato hayo benki” amesema Ismail
Hata hivyo amewasihi Wafanyabiashara wote kuzingatia miongozo inayotolewa na halmashauri na serikali kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kulipia ushuru na kuhakikia wanaopatiwa stakabadhi sawa na kiasi walichotoa kwani kumekuwa udanganyifu kufanyi
Sambamba na hayo katika kipindi hiko cha miezi mitatu wamefuatilia miradi minne yenye thamani ya zaidi ya bilion 7 inayoendelea kutekelezwa na kubaini kasoro ndogo ndogo ambazo wahusika wameshairiwa kurekebisha
Pia wamepokea jumla ya malalamiko 82 Malalamiko yaliyohusu rushwa yaliyokuwa 51 na yasiyohusu rushwa 31 malalamiko hayahusu rushwa hivyo wengine wamwshauriwa kwenda kufungua jalada Mahakamani.
Aidha katika kipindi hicho cha miezi 3 Takukuru ilishiriki kuelimisha vijana walioko ngazi ya vyuo vikuu kuhusu rushwa na dawa za kulevya na uwlimishaji huo ulifanyika kupitia semina warsha pia kupitia vipindi vya TV na redio na Magazeti.