Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed leo amezindua kampeni ya ‘Tuwaambie Kabla Hawajaharibiwa” yenye lengo la kuwaelimisha jamii kuhusu maswala ya ukatili wa kijinsia pamoja na kutoa taarifa kuhusu vitendo vya uhalifu na kuimarisha usalama kwa watoto ndani ya Jamii.

Kampeni hiyo ambayo imeandaliwa na Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma inalenga kuongeza ushirikiano kati ya wananchi na vyombo vya usalama ili kubaini na kuzuia vitendo vya ukatili, wizi, na uhalifu mwingine kabla havijatokea jambo ambalo ni hatua muhimu katika kujenga jamii salama na yenye umoja.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahamed Abbas Ahamed akizindua kitabu cha kampeni yatuwaambie kabla hawajaaribiwa Ruvuma.

Mkuu huyo wa Mkoa Kanali Ahmed alisema kuwa kampeni hiyo ambayo inazungumzia katika mzingira ya shule na vyuo hivyo matarajio yake kwamba itaenda kuwaokoa vijana na kuhakikisha kuwa wale walioanza ngazi zao za masomo wote wanahitimu wakiwa salama na si vinginevyo.

“Tunataraji kuona hawapati ujauzito ,hawaingii kwenye changamoto za madawa ya kulevya lakini tunatarajia kuona wanaondoka hapa wakiwa wamejengeka kimaadili na kiimani”alisema Kanali Ahmed

Alisema kuwa kundi la vijana ni kundi rasmi ambalo kulipata kwake ni rahisi hasa ambao wapo kwenye shule na vyuo lakini pia kuna kundi kubwa ambalo kwa sasa lipo mtaani hivyo waendelee kuongeza mikakati ya kuwafikia ili wanapojenga Taifa lenye vijana wenye maadili basi wasiwaache na wengine nyuma.

Hata hivyo alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa mlezi namba moja wa vijana katika Taifa letu.

Baadhi ya wadau na wanafunzi wa shule za sekondari kutoka Manispaa ya Songea waliohudhuria kampeni ya tuwaambie kabla hawajaaribiwa iliyofanyika katika viwanja vya Michezo vya chuo Cha ualimu Songea.

Alisema kuwa Rais Samia Suluu Hassan katika nyakati tofauti tofauti amekuwa akiwahasa vijana waishi katika maisha yenye maadili mema lakini kubwa zaidi ametambua kuwa moja ya kuwasaidia vijana ni kuwawezesha kupata elimu kwa kuondoa vikwazo vinavyoweza kuwafanya washindwe kuendelea na masomo yao.

Aidha mkuu huyo wa mkoa ameendelea kuwahimiza wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuendelea na zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la mkazi ambalo ndilo linalotoa sifa ya wananchi kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo Oktoba 18 mwaka huu Mkoa huo umefikisha asilimia 67 za waliojiandikisha.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo wa kampeni ya tuwaambie kabla hawajaaribiwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma Odilia Mroso ambaye pia ni Mkuu wa dawati la jinsia Mkoa wa Ruvuma alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuwaelimisha jamii waweze kutambua kwamba kuwepo kwa utandawazi vijana wameharibika imekuwa ni vigumu sana wazazi kuwaletea watoto wao jambo ambalo vijana wamebaki kuleleana wenyewe kwa wenyewe hivyo kupiga tabia ambazo ni mbaya ambazo pia zitaharibu kizazi kijacho na hivyo baadae kukuza Taifa lenye tija.

Kamishna msaidizi mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma Odilia Mroso akieleza lengo la kampeni ya tuwaambie kabla hawajaaribiwa iliyofanyika katika viwanja vya Michezo vya chuo Cha ualimu Matogoro Songea.

“Lengo la kampeni ni kuwaelimisha wajuwe ukatili ni nini,Wajuwe uzalendo,Wajuwe mmomonyoko wa maadili ili kupitia hayo waweze kupambana na matukio ambayo wanakutananayo katika ukatili na kuweza kuyapinga lakini inalenga hasa kupunguza mimba za utotoni mashuleni ,kupunguza rushwa ya ngono kwenye vyuo na tunaamini baada ya kampeni hii kwisha watakuwa na mabadiliko makubwa” alisema Afabde Mroso.

Kwa upande wake John Doto akiwakilisha upande wa mashirika yasiyo ya kiserikali ambaye ni ushauri mkuu wa Afua ya Vijana na jinsia katika mradi wa USAD Afya yangu alisema kuwa wamepokea kampeni hiyo katika Mkoa wa Ruvuma kwa mikono mwili na wamekuwa wakishirikiana na dawati la Jinsia katika kufanya kazi mbalimbali za kuwaelimisha na kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa hiyo kupitia kampeni hiyo itaweka pamoja katika kutoa elimu juu ya ukatili.

Please follow and like us:
Pin Share