Na Tatu Saad,JAMHURI MEDIA

Kocha mkuu wa Yanga SC, Nasreddine Nabi aongeza jicho la uboreshaji katika kikosi cha timu hiyo kwa kuonesha kuvutiwa na mshambuliaji wa AS Real Bamako ya nchini Mali Ousmane Kamissoko.

Kwa mujinu wa taarifa kutoka Yanga, tayari Nabi ameshawataka viongozi wa Yanga SC kuanza mazungumzo mara moja na mshambualiaji huyo.

Nabi amesema kama viongozi watafanikiwa basi ataachana na mchezaji kutoka DR Congo Tuisilia Kisinda kumpisha Ousmane Kamissoko.

“Tunamshukuru sana kocha wetu kwa kuendelea kuwa na jicho la kipekee la kufanya maboresho katika kikosi chetu, pamoja na kuwa bado tuna michezo sita ya kukamilisha msimu huu wa Ligi Kuu, ameuomba uongozi kumfuatilia Mshambuliaji AS Real Bamako, Kamissoko ili kama watafanikiwa kumshawishi aweze kuja akiwa ni mbadala wa Kisinda,” kimeeleza chanzo cha taarifa kutoka Yanga.

Mshambuliaji huyo amekuwa na kiwango bora msimu huu ambapo katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua ya Makundi dhidi ya TP Mazembe, Machi 19 mwaka huu alifunga mabao mawili.