Na Israel Mwaisaka, JakhuriMedia, Nkasi
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Nkasi imempongeza mkuu wa Wilaya Nkasi Peter Lijualikali lwa namna anavyosimamia utekelezaji wa ilani ya CCM .
Pongezi hizo zimetolewa jana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nkasi, Ally Sud Kessy akiwa na kamati ya siasa ya wilaya kwenye ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali wilayani Nkasi.
Amefikia hatua hiyo baada ya kuukagua mradi wa maji Namanyere unaotekelezwa na mamlaka ya maji mjini Namanyere NAUWASA ambapo utekelezaji wake unaenda vizuri na mkuu wa wilaya kuonekana kuufahamu sana mradi huo na hiyo ni kutokana na namna anavyoufuatilia utekelezaji wake.
Kamati hiyo ya siasa licha ya kuukagua mradi huo wa maji pia waliukagua mradi wa ujenzi wa daraja la Kipundukala,ujenzi wa kituo Cha afya Kabwe,daraja la Nangulukulu -Korongwe na mradi wa maji Korongwe unaotekelezwa na mamlaka ya maji mjini na vijijini RUWASA ambapo miradi yote ikionekana kutekelezwa vizuri na kutoa pongezi hizo Kwa mkuu wa wilaya.
Miradi hiyo mingi iliyokaguliwa na kamati hiyo ya CCM ya wilaya mingi ilionyesha itakamilisha mwezi wa 7 kiasi cha mwenyekiti huyo wa CCM kumtaka mkuu huyo wa wilaya aambatane na kamati hiyo ya siasa mwisho wa mwezi wa saba kwenda kufuatilia ukamilishaji wa miradi hiyo kama ilivyohaidiwa kuwa itakua imekamilisha.
Kamati hiyo ya siasa licha ya kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo pia walitoa mapendekezo baadhi ya utekelezaji wa miradi hiyo ili kuweza kuleta tija na kikubwa ni kuhakikisha Wananchi wanapata huduma sahihi katika miradi hiyo.
Sambamba na hilo mwenyekiti huyo wa CCM amewataka wakandarasi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa wilayani Nkasi kuhakikisha kuwa wanaofanya kazi zao kwa weredi Kwa kulinganisha na thamani halisi ya fedha na kwa kufanya hivyo watakua wamemheshimisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DK, Samia Suluhu Hassan ambaye amekua akihakikisha fedha zinakwenda kwenye miradi mbalimbali Ili iweze kuwahudumia wananchi.
DC Lijualikali kwa upande wake aliihakikishia kamati ya siasa kuwa maelekezo yote waliyoyatoa yanatekelezwa na kuwa suala la thamani ya fedha linazingatiwa sana kwenye miradi yote na kuwa atahakikisha miradi yote inakamilika kwa muda sahihi waliokubaliana
Aliendelea kutoa pongezi lwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya Williamu Mwakalambile na watendaji wake kwa namna ambavyo wamekua wakitoa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha utekelezaji wa miradi hiyo unakamilika Kwa wakati na viwango vinavyotakiwa