Na Happy Lazaro,.JamhuriMedia, Hai
Hai.KAMATI ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali (PAC) imetembelea mradi wa kufua umeme wa Kikuletwa uliopo chini ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)wilayani Hai mkoani Kilimanjaro na kueleza kuridhishwa na miradi hiyo ambayo ikikamilika italeta tija kubwa kwa wananchi na wanafunzi katika chuo hicho.
Akizungumzia kuhusu mradi huo Mhandisi msimamizi wa Mkandarasi , Emmanuel Norberts kutoka kampuni ya kichina ya HNAC Technology Co Ltd ambao ndio wanatekeleza mradi huo kwa kushirikiana na kampuni ya wazawa ya Whitecity International Contractors Ltd amesema kuwa mradi huo wa kufua umee umefikia asilimia 20 kwa sasa .

Emmanuel amesema kuwa, mitambo inayotegemewa kutoka nje ipo tayari kwa asilimia 95 ambapo amesema mradi huo utatumika kama kiwanda cha kufundishia wanafunzi wa chuo cha ufundi kwa vitendo hususani wanaosomea maswala ya umeme.
Amesema kuwa ,mradi huo utazalisha megawati 1.65 ambapo umeme mwingine utaingizwa kwenye gridi ya Taifa kwani watauzia Tanesco .
“Mradi huu ulianza rasmi may 14 mwaka jana ambapo unatarajiwa kukamilika.rasmi oktoba 13 ,2025 ambapo umeweza kutoa ajira kwa vijana wazawa 57 kutoka vijiji vya karibu na mradi huu.”amesema Emmanuel.
Naye Mshauri elekezi wa mradi huo ,Injinia Dokta Robert Kabudi amesema kuwa, mradi huo utagharimu USD 4,638,665,32 sawa na fedha za kitanzania zaidi ya Bilioni 11 .

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC)Dokta Mussa Chacha akizungumzia kuhusiana na
Kampasi ya Kikuletwa yenye ukubwa wa ekari 354 ipo kilometa19 kutoka mji wa
Bomang’ombe (Wilaya ya Hai), Mkoani Kilimanjaro.
Amesema kuwa,Kihistoria eneo hili lilijengwa mitambo ya kufua umeme na watawala wa kijerumani miaka ya 1930’ ikiwa na mitambo miwili(2) na ilipofika mwaka1950 uliongezwa mtambo mwingine mmoja.
“Ilipofika mwaka 1970 Shirika la Umeme (TANESCO)walikabidhiwa kiuendeshaji
ambapo kutokanana changamoto mbalimbali Kituo kilisimama uzalishaji wa umeme mwaka1989 ambapo mnamo mwaka 2013 Chuo cha Ufundi Arusha kilikabidhiwa Kituo hiki kwa ajili ya kutumika kwa mafunzo yanishati jadidifu”amesema.

Amefafanua kuwa,malengo makuu ni kutoa
mafunzo,kufanya tafiti mbalimbali kuhusiana na nishati jadidifu na kuzalisha umeme(kama sehemu ya mafunzo–teachingfactory) ambapo kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi naTeknolojia,Chuo kiko katika utekelezaji wa mradi wa EASTRIP unaofadhiliwa na Benki ya Dunia ambapo Kampasi ya Kikuletwa inaendelezwa kuwa kituo cha umahiri katika mafunzo ya nishati jadidifu kikitarajiwa kuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi wasiopungua 643 kitakapokamilika.
Ameongeza kuwa,mchango wake katika kufanikisha malengo makuu ya Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025, na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDPIII)-2021/22- 2025/26 ambapo katika kutekeleza hayo Chuo cha Ufundi Arusha kina majukumu makuu matatu(3) ambayo ni kutoa mafunzo,kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa jamii.
“Chuo kimefanikiwa kununua baadhi ya vifaa na vitendea kazi ikiwemo,magari matatu, vitendea kazi vya ofisini,na kufunga mfumo wa internet.
Aidha ununuzi wa vifaa vya
maabara ya nishati jadidifu kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo(testingnasimulation)
umeshakamilika pamoja na ujenzi wa Miundombinu,Ujenzi wa 11 katika Kampasi ya Kikuletwa umeshakamilika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo,Japhet Hasunga amesema kuwa, wamefurahishwa na mradi wa umeme pamoja na ujenzi wa madarasa na mabweni na dhamani ya hela inaonekana .
“Kwa kweli tumefurahishwa sana na ujenzi wa miradi hii na inaenda vizuri na tumejiridisha namna hela zinavyotumiwa vizuri na ikikamilika italeta tija kubwa sana kwa wanafunzi pamoja na jamii kwa ujumla
“amesema Hasunga.

