Na Lookman Miraji

Kamati ya maendeleo ya bunge la Ulaya limeanza ziara yake nchini hii leo, Februari 25.

Ziara hiyo inafanyika nchini ikiwa na lengo la kuimarisha mahusiano kati ya Umoja wa Ulaya katika suala Zima la maendeleo endelevu.

Kwa mujibu wa ukurasa wa Umoja wa Ulaya nchini imesema kuwa katika siku ya kwanza ya ziara,kamati hiyo imekutana na baadhi ya viongozi waandamizi wa kiserikali na mashirika binafsi nchini.

Taarifa hiyo imesema kuwa kamati hiyo imekutana leo hii na Waziri mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, watoto na makundi maalum, Dorothy Gwajima, Naibu waziri wa mambo ya nnje na ushirikiano wa Afrika mashariki, Cosato Chumi pamoja na asasi mbalimbali za kiraia.