“Hatima ya nchi yetu ni jukumu letu. Kwa pamoja tunaweza kuisaidia nchi yetu kusonga mbele kuelekea kwenye haki zaidi na usawa zaidi kwa Watanzania wote.”
Kauli hii imetolewa kwenye kitabu cha nukuu za Kiswahili za Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere.
***
Teresa – Baraka
“Baadhi ya watu wanakuja katika maisha yako kama baraka, baadhi wanakuja katika maisha kama masomo.”
Kauli hii ilitolewa na Mtawa wa Kanisa Katoliki, Mother Teresa, alizaliwa Agosti 26, 1910, alifariki Septemba 5, 1997.
****
Plato – Kughushi
“Yeyote anayeonekana kwenye kosa la kughushi, hawezi tena kuaminika hata kama anazungumza ukweli.”
Kauli hii ilitolewa na mwanafalsafa Plato katika semina ya Phaedrus. Alizaliwa mwaka 427, Kabla ya Kristo.
Gandhi: Mabadiliko
“Unapaswa kuwa mabadiliko unayoyatamani duniani.”
Haya ni maneno ya mpigania Uhuru wa India Mahatma Gandhi aliyewambia wananchi wa India kuwa mabadiliko hayawezi kutokea bila wao kuwa sehemu ya mabadiliko hayo.