Na Mwandishi Wetu, JakhuriMedia
Jukwau la Wahuriri Tanzunia (TEF) limepokea kwa furaha uteuzi wa Mobhare Matinyi kuwa Mkurugenzi wa ldara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali. Pia TEF inampongeza kwa uteuzi huo wa Oktoba 1, 2023.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na mwenyeliti wa TEF, Deodatus Balile, amwsema kuea TEF tunamshukuru Rais Sumia Suluhu Hassan kwa kufanya uteuzi wa mtu sahihi kushika wadhifa huu, baada ya aliyekuwapo, Gerson Msigwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu.
“Msemaji Mkuu wa Serikali ndiye Mshauri Mkuu wu Masuala ya Habari serikalini. Tunaamini ataifanya kazi hii kwa ustadi wa hali ya juu na kwa ufasaha.
“Wakati tunampongeza Matinyi, tunaomba kumpa sehemu ya ujumbe wa tasnia ya habari kwamba tunayo matarajio halali ya kuwa atakuwa kiunganishi kati yau vyombo vya Haburi na Serikali.
“TEF inamfahamisha Matinyi kuwa pamoja na mumbo mengine, mbele yake kuna uundwaji wa vyombo vinavyoanzishwa kisheria kupitia Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kama ilivyorekebishwa mwaku 2023, jukumu ambalo lilishindikuna tangu mwaku 2016.
“Tunaamini sasa ni wakati mwafaka alisimamie suala hili, ili viundwe.
Kadhalika uchumi wa vyombo vya Habari upo katika hali mbaya, suala linaloathiri ubora wa Habari” amesema Balile.
Serikali ni mnufaika wa Habari zinazochapishwa na kutangazwa na vyombo vya Habari kwa kuwafikishia wananchi uamuzi na utendaji wa siku hadi siku wa Serikali.
Amesema kuwa kutokana na ukweli huu tunaamini ni wakati mwafaka wa Serikali kutenga bajeti ili kuhakikisha vyombo vya Habari vinapata matangazo ya kutosha na kuwa na uwezo wa kiuchumi hali itakayoongeza ubora wa maudhui. Lipo pia la madeni serikalini kwa vyombo vya habari, tunaamini atalifanyia kazi.
“Tunamtakia Matinyi kila la kheri katika nafasi hi na tuna matumaini mak ubwa kwake na tunajua anaweza.
“Sisi kwa upande wetu, tunamhakikishia ushirikiano wa hali ya juu. Hongera sana Matinyi” amesema.