Mkutano wa kilele uliowaleta pamoja wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, SADC, na Jumuiya ya Afrika Mashariki, umeunda jopo la wasuluhishi katika mzozo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kwa mujibu wa tangazo rasmi la kuhitimisha mkutano huo wa kilele uliofanyika usiku wa kuamkia leo, jopo la wasuluhishi lililoteuliwa linajumuisha rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, rais wa zamani wa Afrika Kusini Kgalema Motlanthe, rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba Panza, na rais wa zamani wa Ethiopia Zahle-Work Zewde.Tangazo hilo limeeleza kuwa uteuzi wa jopo hilo umezingatia ukanda, lugha na jinsia.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya SADC, Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, na yule wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais William Ruto wa Kenya ambao kwa pamoja wameuongoza mkutano huo, wamepewa jukumu la kuwakutanisha wapatanishi hao katika muda wa siku saba, kwa ushirikiano na Umoja wa Afrika.
Viongozi wa Jumuiya mbili za kikanda ile ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, SADC na ya Afrika Mashariki, walikutana kwa mara ya kwanza mjini Dar es Salaam mapema mwaka huu kuujadili mzozo wa
Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye nchi yake inatuhumiwa kulisaidia kundi la uasi la M23, ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria mkutano huo uliofanyika kwa njia ya mtandao.
