Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimsikiliza mtaalamu wa kutumia kifaa cha DOZEE kutoka kampuni ya Sakaar Healthtech Limited Yusuph Abdallah aliyekuwa akimuelezea namna kifaa maalumu kijulikanacho kwa jina la DOZEE kinachotumika kufuatilia maendeleo ya mgonjwa anayetibiwa akiwa nyumbani kinavyofanya kazi alipotembelea banda la Taasisi hiyo jana wakati wa Maonesho ya Biashara ya kimataifa ya 48 yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba barabara ya kilwa jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimsikiliza mtaalamu wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alipotembelea banda hilo wakati wa maonesho ya biashara ya kimataifa ya 48 yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba barabara ya kilwa jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa huduma za afya mtandao kutoka kampuni ya cloudscrip Beatrice Mmari akimuelekeza mfanyakazi wa BOT Lameck Kakulu namna ya kujisajiri katika mtandao ili kupata huduma za afya zinazotolewa na JKCI wakati wa maonesho ya biashara ya kimataifa ya 48 yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba barabara ya kilwa jijini Dar es Salaam.
Wananchi waliotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) lililopo katika maonesho ya kimataifa ya 48 ya biashara ya Dar es Salaam wakiwa katika foleni ya kupatiwa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo.