Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inashiriki katika Maadhimisho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yanayofanyika katika viwanja vya Maonesho Mandewa vilivyopo Singida mjini kuanzia tarehe 24 – Aprili 2025.

Katika maonesho haya tunatoa bila malipo huduma za upimaji na matibabu ya  magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya moyo.

Pia tunatoa ushauri wa kiafya kuhusiana na magonjwa ya moyo, elimu ya lishe bora  na ushauri wa magonjwa yatokanayo na kazi.

Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapo hapo na wale watakaokutwa na matatizo yatakayohitaji matibabu ya kibingwa watapewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.

Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0717057478  0745767927.

“Nafasi ya Akili Mnemba na Teknolojia za Kidigitali katika kuimarisha Usalama na Afya Mahali Pa Kazi”.

 Imetolewa na:

Anna Nkinda

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete