JamhuriComments Off on JKCI yaanza kuwahudumia wagonjwa majumbani
…………………………….
Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imeanzisha huduma ya kuwahudumia wagonjwa wakiwa majumbani (home based care) ambayo itasaidia kupunguza gharama ambazo mgonjwa uzitumia akiwa hospitalini.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitagaza huduma hiyo leo Aprili 23, 2024 Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt Piter Kisenge amesema kupitia huduma hii mpya wagonjwa wa moyo watatembelewa na madaktari wakiwa nyumbani .
Dkt Kisenge amesema kupitia huduma hiyo watapewa kifaa kinachoitwa Dozee ambacho kitawekwa chini ya shuka katika kitanda cha mgonjwa.
“Kupitia huduma hii wagonjwa wa moyo wanaohitaji mwendelezo wa matibabu kwa sasa hawatakuwa na haja kufika hospitali kila wakati badala yake watapatiwa huduma hiyo wakiwa nyumbani “amesema Dkt Kisenge
Aidha amesema kifaa hicho kitakuwa kikipima mapigo ya moyo , Oksijeni ya mgonjwa, shinikizo la damu pamoja na kutoa taarifa kwa madaktari.
Aliendelea kueleza kuwa huduma hiyo itasaidia kupunguza vifo vya gafla ambavyo vimekuwa vikiwakumba wagonjwa.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Moyo Dkt Smita Bhalia amesema huduma hiyo pia itatoa elimu ya lishe ,huduma ya Magari ya dharura(Ambulance) pamoja na matibabu ya dawa .