TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inatarajia kuweka kambi maalum ya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo mkoani Dar es salaam na mikoa ya jirani katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani Machi 8, 2024.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano ,Anna Nkinda imesema wataalamu wa JKCI, Hospitali ya Dar Group iliyopo Tazara Wilaya ya Temeke watatoa huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Dk Samia Suluhu Outreach services kwa kufanya kambi hiyo maalum.
“Upimaji huu unafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia tarehe 2 hadi 3,2024 kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 kamili jioni katika hospitali ya JKCI Dar Group.
Aidha amesema katika kambi hiyo kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora ambayo itawapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo ambayo yanayweza kuepukika kwa kuafuata ushauri wa kitaalamu.
“Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mnamatatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0787941606 Dk Samweli Rweyemamu na 0674179036 Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete(JKCI) Hospitali ya Dar Group.
a lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora ambayo itawapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo ambayo yanayweza kuepukika kwa kuafuata ushauri wa kitaalamu.