JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kwa Kamanda wake, Lazaro Mambosasa, leo Desemba 29, 2017 limetoa ripoti yake ya matukio ya kihalifu na oparesheni mbalimbali zilizofanywa na jeshi hilo kwa mwaka 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar, Kamnda Mambosasa amesema matukio ya uhalifu yamepungua kwa kipindi cha januari hadi Desemba 2017 ikilinganishwa na kipindi kama hichio kwa mwaka jana wa 2016 huku akieleza namna ambavyo jeshi hilo limefanikiwa kuwatia mbaroni na kuwafikisha mahakamni watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya kihalifu na jinai.

“Kuanzia Januari hadi Desemba 2017, matukio yaliyoripotiwa kwenye vituo vya Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ni 126,200, wakati mwaka 2016, matukio 129,602 yaliripotiwa. Kati ya hayo, kulikuwa na matukio makubwa ya uhalifu 9,739 wakati mwaka 2016, matukio makubwa 12,550 yaliripotiwa.

“Hali ya amani katika Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, ilikuwa ya kuridhisha kwa mwaka 2017, huku kukiwa na matukio machache ya unyang’anyi wa kutumia silaha ikiwemo wizi wa pikipiki, magari na uporaji ikilinganishwa na mwaka jana.

“Makosa ya jinai mwaka 2017; matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha yalikuwa 127, ulawiti 48, unyang’anyi wa kutumia nguvu 838, uvunjaji 3,695.

“Oparesheni maalum mwaka 2017; silaha 27 zimekamatwa, risasi 1,147, SMG 2 na risasi 824, bastola 15 na risasi 127, shotgun 6 na risasi 394, rifle 4 na risasi 263 na watuhumiwa 25 wa silaha hizo. Majambazi sugu 36 walikamatwa, magari ya wizi 213, yaliyopatikana ni 32, pikipiki zilizoibiwa ni 1,778, zilizopatikana ni 127.

“Matukio barabarani mwaka 2017; ajali zilizosababisha vifo 182, waliofariki ni 194, waliojeruhiwa ni 1,917, ajali za pikipiki ni 514, vifo vya pikipiki ni 63, waliojeruhiwa ni 369,”