Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ‘limedungua’ ndege sita zisizo na rubani za Kamikaze za Jeshi la Rwanda katika mji wa Mambasa eneo la Lubero katika Mkoa wa Nord Kivu.
Msemaji wa Jeshi Lt Kanali Mak Hazukay alisema waasi wa M23 walikuwa wakiwatumia vijana waliovalia sare za kijeshi za Rwanda kama ‘wale wa ziada’ katika maeneo ya vita.
“Jeshi linatoa wito kwa raia wanaotumiwa kama ngao kusalimisha silaha zao, na linawataka wakazi wa maeneo yanayokaliwa kuondoka kwenye kwa usalama wao,” Hazukay alisema.
Lubero imekuwa kitovu cha mapigano mapya kati ya waasi na vikosi vya usalama baada ya mazungumzo kati ya DR Congo na Rwanda hivi karibuni kushindikana.
Jeshi la Congo na waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda wamekuwa wakishambulizi mara kwa mara lakini Rwanda imekuwa ikikanusha kuunga mkono waasi wa M23 na kuishtumu serikali ya Congo kushirikiana na waasi wa Rwanda wa FDLR shutuma ambazo pia Congo inakanusha.