JESHI la Israel lilitangaza siku ya Jumatano kuwa wanajeshi wake sita waliuawa katika mapigano kusini mwa Lebanon.
Hii inaleta idadi ya wanajeshi waliouawa katika vita na Hezbollah tangu kuanza kwa mashambulizi ya ardhini kwenye ardhi ya Lebanon mnamo Septemba 30 kufikia 47.
Jeshi lilichapisha majina ya wanajeshi watano waliouawa katika vita hivi, huku jina la mwanajeshi wa sita likiwa bado linasubiri kuidhinishwa kuchapishwa, kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Israel.
Alisema mapigano hayo yalidumu kwa saa 3, kuanzia saa 10 asubuhi hadi saa 1 jioni
Redio ya Jeshi la Israel ilifichua kuwa mapigano hayo yalijumuisha mashambulizi mawili ya kuvizia, moja ndani ya jengo hilo na jingine nje yake, kwa makombora ya kukinga vifaru.
IDF ilitangaza kuuawa kwa wanajeshi na maafisa 107 kutoka Brigedi ya Golani tangu Oktoba 7 mwaka jana.
Alisema uondoaji wa askari waliojeruhiwa na waliokufa ulikuwa mgumu na jeshi “linahitaji muda” kuelewa sababu ya tukio hilo.
Alidokeza kuwa kuna imani kwamba kuna shimo ndani ya jengo ambalo liliruhusu wapiganaji wa Hezbollah kutojeruhiwa licha ya kushambuliwa kwa bomu.