Jana Septemba 6,2024 zilisambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii ikieleza kuwa jioni maeneo ya Tegeta Jijini Dar es Salaam, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ally Mohamed Kibao, akiwa safarini na basi la Tashrif alichukuliwa na kushushwa toka kwenye basi hilo na watu ambao hawakuweza kujulikana majina yao.

Aidha, leo Septemba 7,2024 tumesikia taarifa kuhusiana na tukio hilo kupitia vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo John Mnyika.

Jeshi la Polisi, lingependa kutoa taarifa kuwa, lilipokea taarifa hiyo na kuanza uchunguzi wa kubaini kilichotokea, chanzo chake na watu waliohusika ni akina nani.

Please follow and like us:
Pin Share