Pambano la fainali la kombe la Mapinduzi limezidi kuvuta hisia za mashabiki wa soka visiwani Zanzibar baada ya makocha wa timu zote mbili kutambiana
TIMU za Azam na URA keshozitashuka Uwanja wa Amaan Zanzibar kusaka taji la 12, la michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Timu hizo mbili zinakutana kwa mara ya pili kwenye michuano ya mwaka huu mara ya kwanza zilikutana kwenye hatua ya makundi na Azam kupoteza
mchezo kwa bao 1-0.
Mchezo wa fainali unatarajiwa kuwa mkali kwasababu pande ote mbili zimejipanga hasa wenyeji Azam ambao niwazi hawatokubali kupoteza
mchezo kwa mara ya pili mbele ya timu hiyo kutoka Uganda.
Azam ambao ndiyo mabingwa watetezi, wamedhamiria kulibakiza taji hilo kwenye aridhi ya Tanzania kwa kuhakikisha wanalipa kisasi na kushinda
mchezo huo licha ya ugumu wa wapinzani wao URA.
Kuelekea kwenye mchezo huo kocha Arisitca Cioaba wa Azam FC, amesema kikosi chake kipo imara kuhakikisha wanashinda mchezo huo na
kulibakiza taji la Mapinduzi kwenye aridhi ya Tanzania.
Kocha huyo raia wa Romania, amesema anawajua vizuri wapinzani wao URA, na hadhani kama wana nafasi ya kuwafunga tene kutokana na umuhimu wa
mchezo wenyewe pamoja na mikakati aliyojiwekea na wachezaji wake.
“Nimchezo mgumu na mzuri kwa timu zote mbili ambao mwisho wake Azam ndiyo watakaokuwa mabingwa kwasababu nimewasoma vizuri URA na sizani
kama wanaweza kutusumbua tena kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa kwanza,” amesema Cioaba.
Tegemeo kubwa kwa kocha huyo ni kipa Razak Abalora ambaye ameonyesha uwezo mkubwa na mshambuliaji Bernald Authur anayefanya kazi kubwa ya
kuwasumbua mabeki wa timu pinzani huku Paul Peter, Idd Kipwagile na Shabani Idd wakicheka na nyavu
Kwaupande wake kocha wa URA Ntaka Paul, amesema fainali ya kesho ni nyepesi kwake kwasababu timu anayokwenda kucheza nayo anaifahamu
vizuri na anajua wapi pakuwadhibiti ili wasiwe na madhara kwake.
Nkata alisema kama haki itatendeka kwenye mchezo huo anahakik timu yake ndiyo itaibuka na ushindi kama ilivyokuwa mwaka 2016,
walipoifunga Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa fainali ya michuano hiyo.
Kocha huyo amesema kikosi chake cha kesho hakitakuwa na mabadiliko makubwa sana na asilimia kubwa ya wachezaji itakuwa ni ileile
akiwategemea zaidi Moses Sseruyide Jimmy Kalaba, Bokota Labama na Shafik Kagimu.