Na Dotto Kwilasa, Jamhurimedia ,Dodoma
Asilimia 66 ya watoto kuanzia umri wa siku 0 hadi miaka 8 katika jangwa la Sahara wanakabiliwa na kutokuwa na utimilifu wa akili jambo ambalo linaweza kusababisha kuwa na watu ambao hawawezi kuwa na uhakika wa uzalishaji huku asilimia 47 tu ya watoto wenye umri huo ndio wenye utimilifu wa akili.
Hayo yamesemwa na Mratibu Mradi wa Watoto wetu Mkoa wa Dodoma ambaye alimwakilishi Mkurugenzi wa Children in Cross Fire,Bw. Frank Samso,kwenye mafunzo ya Kitaifa ya Sayansi ya Malezi na Maendeleo ya awali ya mtoto yanayofanyika jijini Dodoma, ambayo yanadhaminiwa na mradi wa Mtoto kwanza kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum.
Samson amesema kuwa ili kuwa na Taifa Bora ni lazima kuwekeza katika akili ya mtoto akiwa na umri wa kuanzia siku 0 hadi mika 8 kwa lengo la kuokoa kizazi cha watoto wanaozaliwa katika jangwa la Sahala na kwa taifa jambo ambalo linaweza kuchochea uchumi wa nchi kwa kuwa na watu wenye utimilifu wa akili katika uzalishaji.
“Ukimwandaa mtoto kiakili kwa kuanzia Umri wa siku 0 hadi miaka 8 utakuwa umewekeza kwa mtoto kwa asilimia 96 jambo ambalo litawezesha taifa kuwa na watoto wenye akili na wenye uwezo mkubwa wa uzalishaji kutokana na kuwa na utimilifu wa akili bora ukilinganisha na watoto ambao watakuwa hawajaandaliwa vyema katika utimilifu wa akili” alieleza Mwakilishi wa Cross fire.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtandao wa Makuzi ya Mtoto Tanzania TECDEN Mwajuma Rwebangila ni kati ya kundi lililoingia mkataba nchi nzima kwa kuwezesha maboresho ya malezi ya mtoto na kuongeza utaalamu kwa wataalamu kitaifa kwa kufanya mafunzo kikamilifu kutoka kwa watoto asilimia 26 hadi kufikia asilimia 53 kwa utimilifu wa akili.
Aidha ameeleza kuwa mtandao huo umekuwa ukihamasisha zaidi jamii kujua umuhimu wa kuwepo kwa uboreshaji wa marezi na makuzi kwa watoto kwa lengo la kupata watoto wenye timilifu wa akili kwa lengo lakuwa na taifa bora na lenye kuwa na wazalishaji wenye tija badala ya kuwa na jamii kubwa yenye kuwa na wazalishai wachache.
Naye Mwakilishi wa chuo kikuu cha Aghakani kutoka nchini Kenya Prof. Amina Abubakari amesema kuwa yeye akiwa mwadhili kutoka chuo hicho anayo amani kubwa ya kushirikiana na wataalamu wa kulinda maendeleo ya watoto nchini Tanzania jambo ambalo alisema kuwa ni njia pekee ya kuwezesha kizazi cha umri huo kuwa imara katika utimilifu wa akili lakini pia jamii kutambua umuhimu wa kulinda na kuzingatia malezi ya mtoto .
“Tunatakiwa kuwapatia mafunzo watoto wetu wenye umri kuanzia siku 0 hadi kufikia miaka 8 kwa lengo la kuwa na kzazi imara na chenye uwezo mkubwa wa kufikiri kwa mapana jambo ambalo ameeleza kuwa linaweza kusababisha kuwepo kwa mageuzi makubwa ya kiuchumi jambo ambalo linafanya kuwepo kwa uhakika wa kuwa na watu wa taifa sahihi zaidi” alisema Prof.Amima.
Awali Akifungua mafunzo hayo Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum, Mwanahidi Ally Khamisi amesema kuwa mafunzo hayo yanataka kufanywa kwa uaminifu mkubwa na uadilifu ili kuhakikisha elimu hiyo inapelekwa kwa ngazi zote.
“Serikali kwa kutambua umuhimu wa kukuza utimilifu wa akili ya mtoto itahakikisha inaendelea kutenga bajeti kwa lengo la kutoa elimu kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa kwa lengo la kuhakikisha inatokomezwa hali ya kuwa na watoto wasiokuwa na utimiligu wa hakili na badala yake kuwa na watoto wenye utimilifu wa akili kwa nia ya kupata taifa lenye watu wenye ueledi na wanaoweza kuzalisha kutokana na kuwa na hakili zilizo sawa zaidi.