Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akisalimiana na watumishi wa Mahakama ya wilaya ya Nzega alipowasili kukagua shughuli za Mahakama. Jaji Mkuu ameanza ziara ya kikazi katika mkoa wa Tabora na Kigoma ambayo ni Kanda ya Tabora
Jajki Mkuu akizungumza
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngulupa akimpokea Jaji Mkuu alipowasili ofisini kwake Nzega
Mkuu wa Wilaya ya Nzega akizungumza
Jaji Mkuu akimkabidhi Mkuu wa wilaya kitabu kinachoelezea Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Jarida la Mahakama alipofika ofisini kwake kumtembelea
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo nchini kusimamia mabaraza ya kata yaliyoanzishwa kwa Shjeria yam waka 1985 kwa kuwa mabaraza hayo ni sehemu muhimu katika mfumo wa utoaji haki kutokana na kazi yake ya kusuluhisha na kupatanisha mashauri madogo madogo ya jinai na madai.
Akizungumza na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga na Nzega pamoja na Mahakama ya Mwanzo ya Ziba na Nyasa mkoani Tabora, Jaji Mkuu amesema mfumo wa utoaji haki kupitia mabaraza ya kata unawaunganisha wananchi tofauti na pale kesi inaposikilizwa Mahakamani ambapo mar azote aliyeshindwa hujenga uadui na aliyeshinda.
Jaji Mkuu amesema endapo mabaraza ya Kata yatasimamiwa ipasavyo ni wazi kuwa idadi ya kesi zinazofunguliwa kwenye Mahakama za Mwanzo nchini itapungua kwa kiasi kikubwa kwa kuwa kesi nyingi zitaamuliwa kwenye mabaraza hayo kwa njia ya usuluhishi na upatanishi. Aliongeza kuwa kesi zote zinazosajiliwa nchini asilimia 74 ni za Mahakama za Mwanzo.
Amesema ili kuimarisha mfumo wa utoaji haki kupitia mabaraza ya kata, Mahakama ya Tanzania imeandaa mpango wa mafunzo utakaowakutanisha Mahakimu pamoja na wajumbe wa mabaraza ya kata.
Aidha, Prof. Juma amewataka watumishi wa Mahakama kuzingatia maadili ya kazi na kutoa haki kwa wakati kwa kuwa kwa kufanya hivyo watachangia katika kukuza uchumi wa Taifa.
Amesema mashauri yanapomalizika kwa wakati hutoa nafasi kwa wananchi kufanya shughuli za uzalishaji wa mali na hivyo kukuza uchumi wa taifa kwa ujumla.
“Mnapofanya kazi ya utoaji wa haki mjisikie ni sehemu ya kujenga uchumi maana bila ya haki hakuna amani”, alisema Prof. Juma na kuongeza kuwa Mahakama ina mchango mkubwa katika kudumisha Amani, utulivu na umoja ambayo ni sehemu ya Dira ya Taifa yam waka 2025.
Akizungumzia matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ndani ya Mahakama, Jaji Mkuu amesema tayari Mahakama imeshaanza kutumia mfumo huo kwa kukusanya takwimu za mashauri kuanzia ngazi ya Mahakama za wilaya na pia baadhi ya majengo ya Mahakama tayari yanatumia TEHAMA huku akitolea mfano jingo la Mahakama Kuu kanda ya Mbeya na kituo cha Mafunzo Kisutu.
Amewataka watumishi wa Mahakama wa kada zote kujiendeleza hasa katika matumizi ya Tehama ili Mahakama iytekeleze wajibu wake wa kutoa haki kwa wakati. Amesema, kupitia Tehama mahakama itatoa haki kwa haraka na kwa wakakti hivyo wananchi wataongeza Imani yao kwa mhimili huo.
Mahakama katika katika wilaya za Nzega, Igunga pamoja na Mahakama za Mwanzo Jaji Mkuu wa Tanzania ameanza ziara ya kikazi Mahakama Kuu kanda ya Tabora ambayo inajumuisha mikoa ya Tabora na Kigoma. Leo amekagua shughuli za za Ziba na Nyasa zilizopo mkoani Tabora.