Jaji Mkuu, Prof Ibrahimu Juma, akizungumza jambo katika hafla hiyo.

Baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo.

Prof Juma akizungumza na waandishi wa habari.

…Akiwa na majaji katika picha ya pamoja.

JAJI Mkuu  Prof Ibrahimu Juma amefungua mafunzo elekezi kwa majaji wapya 14 wa Mahakama Kuu nchini yenye lengo la kuwataka wafanye kazi kwa umakini.

Mafunzo hayo ni ya wiki tatu na yatakuwa katika Kituo cha Mahakama cha Mafunzo ya Uongozi kilichopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Akizungumza katika hafla hiyo Prof. Juma amesema kuwa majaji wanatakiwa kufahamu wananchi wanavyozitambua haki zao za msingi na hivyo  wasikilize kesi zilizopo  na kuzitolea uamuzi kwa wakati.

Kuhusu mlundikano wa kesi, amewataka majaji hao kujitahidi kuamua kesi ambazo zinaweza kutolewa uamuzi mapema na kumalizika, kwani jaji mmoja anaweza kuwa na kesi zaidi ya 400.