JamhuriComments Off on Jafo awakumbusha Watanzania kutunza mazingira
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo, akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuongoza zoezi la upatandaji miti lililoandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa hilo.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo, amewataka Watanzania nchini kuendelea kutunza mazingira ili kukabilina na athari za mabadiliko tabianchi ambazo zinatishia uhai wa viumbe hai kutokana na ukame mkali uliopo hivi sasa katika maeneo mengi ya nchi.
Waziri Jafo, ameyabainisha jijini Dodoma mara baada ya kushiriki tukio la upatandaji miti lililoandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa hilo.
Dkt.Jafo ameeleza kuwa hivi sasa dunia imekubwa na athari kubwa za kimazingira ambazo zinatokana na mabadiliko tabianchi hali ambayo kila mtu anapaswa kutimiza wajibu wake katika kutunza na kuhifadhi mazingira.
“Hivi sasa ni mwezi Juni ni muda machache sana tangu kuisha kwa mvua za masika lakini ukitembea katika maeneo mengi ya nchi ni makame kwelikweli hii inaonyesha kuwa hadi itakapofika mwezi Novemba hali itakuwa mbaya sana’alisema Jafo
Aidha, amesema mabadiliko tabianchi yameathiri maeneo mengi nchini ikiwemo kukauka kwa vyanzo vya maji hali ambayo inatishia uhai wa mifugo na viumbe vingine.
“Hivi sasa athari za kimazingira zimeathiri hata bahari kina cha maji kinaongezeka nemba Pemba nenda Unguja kuna maeneo ambayo yalikuwa makavu hivi sasa maji yanaongezeka hii yote ni kutokana na kuongezeka kwa joto duniani barafu zinayeyuka hivyo hali hii inatulazimu kuhakikisha kila mtu natunza mazingira kwa nguvu zake zote”amefafanua Jafo
Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la KKKT, Dayoyosi ya Dodoma Christian Ndosa, ameeleza lengo la kuandaa tukio la upanadaji miti ni kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na serikali ya awamu ya sita katika kutunza mazingira na kukabilina na mabadiliko tabianchi.
Askofu Ndosa, amesema katika maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa hilo hilo mwaka huu wamepanga kupatanda miti 30,000.
“Tumenga kupanda miti 30,000 na leo tunaanza na miti 1,000 na zoezi hili litaendelea katika maeneo mengine ya Dayosisi yetu ili kuhakikisha tunapanda miti ya kutosha ili kukabiliana na mabadiliko tabia nchi”alisema
Naye Makamu mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Maji na Mazingira Anna Lupembe, ametoa wito kwa makanisa kuunga mkono jitihada za serikali kwa kupanda miti katika maeneo yao yote ya wazi.