Mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Colombia, Ivan Dukee amewahutubia wafuasi wake mjini Bogota. Bwana Dukee, mwenye umri wa miaka 41,aliahidi kufanyia marekebisho mkataba wa amani uliyofikiwa kati ya serikali na wapiganaji wa FARC.

Alijizolea asilimia 54 ya kura ikiwa ni asilimia kumi na mbili zaidi ya mpinzani wake,Gustavo Petro ambaye ni mpiganaji wa zamani.

Bwana Duque anatajwa kuwa ni chaguo la wafanyabiashara kwa sababu anataka kupunguza na kuongeza uwekezaji na kuongeza thamani ya fedha.

Hata hivyo matokeo hayo bado yanaacha swali lisilo na jibu kama utawala mpya wa Duque kama utakomesha kundi la wapiganaji wa Farc.

Duque anayeungwa mkono na rais wa zamani Alvaro Uribe, amesema kuwa atafanyia marekebisho makubaliano yam waka 2016 ambao uliwapatia waasi wa nafasi ndani ya Congress.