Israel imesitisha usambazaji wa umeme katika Ukanda wa Gaza huku ikijaribu kuishinikiza Hamas kukubali kuongezwa muda wa awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano.

Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas kimsingi yalimalizika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Athari za hatua hiyo bado hazijajulikana. Lakini, mitambo ya kuondoa chumvi kwenye maji ya kunywa ya eneo la Gaza hutegemea nguvu za umeme wa Israel.

Eneo hilo limeharibiwa kwa kiasi kikubwa na kampeni ya kijeshi ya Israeli tangu shambulizi la Oktoba 2023 na baadhi ya wasambazaji wamekuwa wakisambaza umeme kwa kutumia majenereta na nguvu ya jua.

Kundi la Hamas limetoa wito wa kuanza mara moja kwa awamu ya pili ya makubaliano ya kusitisha mapigano, ambayo yanalenga kupata suluhisho la kudumu la mapigano hayo.