Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz amekiri Israel  kuhusika na mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh mjini Tehran mwezi Julai.

Israel Katz alitoa maoni hayo katika hotuba yake akiahidi kuwalenga wakuu wa vuguvugu la Houthi linaloungwa mkono na Iran nchini Yemen, ambalo limekuwa likirusha makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya Israel.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema baadhi ya hatua zimeanza kuchukuliwa katika kukubaliana kusitisha mapigano huko Gaza na Hamas  lakini hakuweka bayana lini makubaliano hayo yataafikiwa.