Mamlaka ya ulinzi wa anga ya Israel imesema imefanikiwa kulizuia kombora ambalo limefyatuliwa kutoka Yemen.

Asubuhi ya mapema ya jana ving’ora vya mashambulizi ya anga vilisikika karibu na Tel Aviv na katika maeneo mengine. Tovuti ya habari ya Israel ynet iliripoti kuwa milio hiyo ilisababishwa na kombora la balestiki.

Na jeshi likasema lilizuiwa kabla ya kuingia katika ardhi ya Israel. Na wakati kila upande ukiwa katika makubaliano ya kusitisha mapigano, Hezbollah, mshirika wa Iran huko Lebanon, wanamgambo wa Houthi wa Yemen, ambao pia wanaungwa mkono na Iran wametishia kufanya mashambulizi zaidi dhidi ya Israel.

Wanasema uungaji mkono wao unaendelea kwa Wapalestina katikaUkanda wa Gaza, ambapo Israel imekuwa ikiendesha vita dhidi ya wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas tangu shambulio la Oktoba 7, 2023 katika ardhi ya Isreal.