Alizaliwa katika kambi ya wakimbizi huko Gaza mwaka 1963, Ismail Haniyeh alikuwa mwanachama muhimu wa Hamas tangu kuanzishwa kwake.

Alifungwa na Israel mara kadhaa na wakati fulani alifukuzwa kwenda kuishi Lebanon kusini kwa miezi sita.

Mnamo 2003, alinusurika jaribio la mauaji la Israeli, pamoja na mwanzilishi wa Hamas.

Miaka mitatu baadaye, alikuwa waziri mkuu wa Palestina kwa muda mfupi baada ya Hamas kushinda uchaguzi – lakini mpasuko mkali kati ya Hamas na kundi lingine kuu la Wapalestina, Fatah, ulifuata mwaka mmoja baadaye.

Akizingatiwa sana kama muelewa wa uhalisia wa mambo, Haniyeh alisemekana kudumisha uhusiano mzuri na vikundi vingine hasimu vya Palestina.

Alichaguliwa kuwa mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas mwaka 2017. Katika miaka ya hivi karibuni, aliishi uhamishoni, akiishi Uturuki na Qatar.

Alikuwa akitekeleza jukumu muhimu katika mazungumzo juu ya mpango wa kusitisha mapigano huko Gaza.