Iran imetangaza likizo ya siku mbili kwa wafanyakazi wa Serikali na benki kutokana na hali ya joto inayoongezeka kote nchini humo.

Uamuzi huo umewadia wakati nchi duniani kote, ikiwa ni pamoja na Iran, zinakabiliwa na ongezeko la joto la kihistoria na ambalo halijawahi kutokea.

Ofisi ya hali ya hewa ya Iran ilitabiri joto linaweza kuwa kati ya nyuzi joto 40 na 50 katika miji mingi.

Miji, ikiwa ni pamoja na majimbo ya Ilam, Bushehr na Khuzestan, imerekodi viwango vya joto kuongezeka zaidi ya nyuzi joto 45 hivi karibuni, kama ilivyoripotiwa na chombo cha habari cha Iran kinachomilikiwa na serikali, IRIB.

Dehloran, mji ulioko magharibi mwa Iran, ulirekodi joto la juu zaidi la nyuzi joto 50 nchini Iran katika muda wa saa 24 zilizopita huku wizara ya afya ya Iran ikiendelea kutoa maonyo kuhusu kiharusi cha joto kutokana na kupigwa na jua kupita kiasi