Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema Marekani itapata pigo kubwa ikiwa itatekeleza tishio la kuishambulia kwa mabomu Iran ikiwa haitafikia makubaliano mapya ya nyuklia na Marekani.
Kiongozi huyo mkuu wa Iran amesema ikiwa Marekani inafikiria kuleta uchochezi ndani ya nchi hiyo kama ilivyokuwa miaka iliyopita, raia wa Iran watakabiliana nayo.
Iran yakataa kuingia katika mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani kuhusu mpango wake wa nyuklia
Hapo jana, Trump alisisitiza tishio lake kwamba Iran itashambuliwa kwa mabomu ikiwa haitakubali pendekezo lake la mazungumzo yaliyoainishwa katika barua iliyotumwa kwa uongozi wa Iranmapema mwezi Machi, na kuipa nchi hiyo muda wa miezi miwili kufanya uamuzi.
