Mamlaka ya usafiri wa anga nchini Iran imeruhusu mashirika ya ndege kuanza kupanga ratiba ya safari zake za ndege baada ya kujiridhisha usalama wa anga upo.
Kwa mujibu wa Msemaji wa mamlaka ya usafiri wa anga amesema safari zote za ndege awali zilifutwa kutokana na vikwazo vya kiutendaji.
Wakala wa usalama wa anga wa Umoja wa Ulaya umeyashauri mashirika ya ndege ya Ulaya kuepuka anga ya Iran angalau hadi Oktoba 31, wakati wakiendelea kutathmini hali ya usalama wa anga.
Iran iliamua kusitisha safari zote za ndege Jumanne iliyopita baada ya kuvurumisha makombora kuelekea Israel katika shambulio ambalo serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu imeahidi kujibu mashambulizi.